Umiliki
Kutoa ushauri kuhusu usimamizi wa Miliki za Serikali, kutwaa na kuendeleza ardhi, uundaji wa sera mbalimbali za ndani za makazi ya Serikali, kanuni na taratibu, za utoaji wa huduma za tathmini ya makazi ya Serikali.
Ushauri
Kutoa huduma ya ushauri kwa miradi ya majengo ya Serikali. Kuidhinisha michoro ya ujenzi ya Taasisi za Serikali na kutoa vibali vya ujenzi wa majengo ya Serikali.
Miradi
Kutoa ushauri kuhusu usimamizi wa Miliki za Serikali, kutwaa na kuendeleza ardhi, uundaji wa sera mbalimbali za ndani za makazi ya Serikali, kanuni na taratibu, za utoaji wa huduma za tathmini ya makazi ya Serikali.
Ujenzi
Wakala wa Majengo ZBA hutoa huduma za Ujenzi , ukarabati ,usimamizi wa Nyumba na Majengo mapya ya Serikali
Mkurugenzi Mtendaji
Ndg Kassim Mussa Issa
Wakala wa Majengo -ZBA
Wakala wa Majengo Zanzibar ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mamlaka ya Rais wa Zanzibar chini ya kifungu nambari 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu nambari 55 cha Sheria ya Utumishi wa Umma Nambari 2 ya mwaka 2011, kupitia tangazo la kisheria (Legal Notice) nambari 50 la tarehe 12 Mei, 2017.
Wakala wa Majengo Zanzibar ilianzishwa kwa malengo ya kuimarisha usimamizi wa majengo ya Serikali na kuwapatia makazi yaliyo bora na nafuu viongozi na watumishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Vile vile, Wakala inawajibu wa kuratibu na kusimamia shughuli zote za ujenzi wa majengo ya Serikali kwa Unguja na Pemba na kufanya matengenezo ya majengo hayo ya Serikali na kuhakikisha ubora na viwango vya ujenzi vinafikiwa.