Dira
Kuwa taasisisi bora na yenye ufanisi ambayo itahakikisha upatikanaji wa majengo bora na ya kisasa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dhamira
Kujenga, kushauri, kusimamia na kufanyia ukarabati majengo ya Serikali ili kuipatia serikali majengo bora na ya kisasa pamoja na kuwapatia nyumba bora na nafuu viongozi wa SMZ na watumishi wa umma kwa ujumla.
Misingi Mikuu
- Kuhamasisha na kushajihisha maendeleo na utanuzi wa majengo ya Serikali.
- Kujenga, kukodisha na kuweka thamani ya majengo ya Serikali katika bei nafuu au kukopesha kwa watumishi wa umma.
- Kuendeleza na kuanzisha njia za uendeshaji na kusimamia makazi ya watumishi wa umma.
- Kufanya tafiti zinazohusu masuala ya ujenzi.
- Kutoa huduma za kiushari kwa kuzingatia malengo na kazi za Wakala.
- Kuanzisha na kuendeleza mfumo wa takwimu wa majengo ya Serikali (Public Building Data Base)
- Kuwa msimamizi (Custodiun) na muendeshaji (Operator) wa Majengo yote ya Serikali
- Kupanga ujenzi wa majengo ya serikali kulingana na mahitaji.
- Kushauri na kupendekeza kwa Waziri juu ya masuala yanayoshabihiana na malengo ya Wakala
- Kufanya kazi nyengine zote zitakazo leta ufanisi katika utekelezaji wa kazi za Wakala bila kuvunja Sheria iliyoanzishwa kwake.